MAJI NI UHAI
Kunywa maji
safi na salama kwa kiasi kinachostahili kiafya kunaweza kuyaboresha
maisha yako na kukufanya ujihisi mwenye afya na furaha zaidi .
Kunywa maji ya kutosha kuna faida nyingi. Tukichukulia kunywa maji ya
kutosha ni mithili biashara kati ya wewe na afya yako, biashara hii
inalipa.
Zifuatazo ni baadhi ya faida za kunywa maji ya kutosha .
- kusaidia mmeng'enyo wa chakula.
Vimengenya na Kemikali mbalimbali zinazohusika na mmen'genyo au usagaji
wa chakula mwilini ziko katika hali ya mchanganyiko na maji. Ili hivi
viweze kufanya kazi vizuri inatakiwa kuwe na uwiano sahihi kati yake na
maji.Pia maji yanahusika katika kulainisha baadhi ya vyakula . Pia kunywa maji ya kutosha kunaongeza ufanisi wa mwili katika kusharabu chakula.
- Dawa ya maumivu ya kichwa.
Mara
nyingine maumivu ya kichwa yanasababishwa na upungufu wa maji mwilini.
Hii inamaanisha, kama una maumivu ya kichwa yanayosababishwa na upungufu
wa maji mwilini unaweza kughairi kumeza vidonge vya kutuliza maumivu na
kunywa maji. Hii inawezekana kwenye baadhi ya maumivu ya mgongo pia.
Pendezesha ngozi yako kwa kunywa maji ya kutosha. Unaweza
kuboresha sura na mguso wa ngozi yako kwa kunywa maji ya kutosha kwani
maji yanasaidia kuboresha tishu za ngozi na kuongeza unyevu kwenye ngozi
.
Maji
yanauweka ubongo katika hali nzuri zaidi na ya ufanisi zaidi. Kunywa
maji ya kutosha kunamwezesha mtu kufikiria kwa ufanisi zaidi.
- kutatua tatizo la kukaukiwa haja kubwa (constipation)
Sehemu
kikubwa ya haja kubwa ni maji. Kunywa maji ya kutosha kunaweza
kukusaidia kupata haja kubwa kiulaini na mara kwa nyingi zaidi.
- kuboresha hali ya viungo na misuli
Maji ya kutosha yanasaidia kupunguza tatizo la kubanwa misuli na pia hupunguza msuguano katika viungo vyako.
Maji yanachochea shughuli za kimetaboliki mwilini na kuongeza ufanisi wa ubongo kwa hiyo yanapunguza uchovu.
- kupunguza uwezekano wa kupata baadhi ya magonjwa.
Uwezekano wa kupata mafua,mawe ya figo,matatizo ya ini,baadhi ya saratani n.k unaweza kupunguzwa kwa kunywa maji ya kutosha .
- Maji yanaweza kusaidia katika kupunguza uzito.
Kama
uko katika mkakati wa kupunguza uzito maji yanaweza kukusaidia kwa
kiasi kikubwa. Maji huongeza kasi ya shughuli za kimetaboliki mwilini.
Ongezeko hilo la kimetaboliki
husababisha mwili kutumia nishati nyingi zaidi na hivyo huweza kupunguza
kiasi cha nishati ambacho kitahifadhiwa mwilini katika hali ya mafuta
au kupunguza kiasi cha nishati
kilichohifadhiwa mwilini.Pia ongezeko la ufanisi wa figo na ini kutokana
na kunywa maji ya kutosha husaidia kutoa mazao ya mafuta ya ziada
mwilini.
Maji hayaongezi nishati mwilini, kwa hiyo unywapo maji badala ya
juisi,soda au vyakula au vinywaji vingine ambavyo huongeza nishati au
mafuta mwilini unaongeza uwezekano wa kupungua uzito.
kunywa
maji ya kutosha kutakufanya ujisikie vizuri na pia kunaweza kupunguza
safari za hospitali. Kunywa maji ya kutosha, fanya siku yako iwe poa
zaidi
No comments:
Post a Comment
HTML tags