Wednesday, August 10, 2011

Ugonjwa wa wengi

Inafahamika kuwa watu wengi wana tabia ya kung'ata kucha ...


Sababu kuu zinazopelekea mtu kung'ata kucha
  • Msongo wa mawazo (Stess) 
  • Woga hasa pale anapotakiwa wanatakiwa kufanya vitu vikubwa
  • Kukosa kitu cha kufanya (Boredom) 
  • Kutokuwa Comfortable tukio linaloendelea au na wakati ulionao 


Madhara ya kung'ata kucha
  • Kuhamisha bacteria kutoka vidoleni mwako kwenda mdomoni
  • Mizizi ya meno kulegea hasa kama kucha ni ngumu sana
  • Kutoka damu kuzunguka vidole
  • Vijinyama kuchomoza pembeni ya vidole
  • Vidole kuvimba na kutunga usaha hata kusababisha maumivu makali 

Kuacha kung'ata kucha si jambo rahisi ,ila kama umeshachoshwa na maumivu , kutokwa na damu kuzunguka kucha zako, jaribu  kufanya yafuatayo yanaweza kukusaidia kuacha tabia hiyo na kufanya kucha zako  ziwe za kupendeza


*Hakikisha muda wote mikono yako ina kazi ya kufanya ama imeshikilia kitu iyo itakusaidia usipate nafasi ya kung'ata kucha

*Muda wote paka rangi ua hina vidole vyako ili pindi utakapotaka kung'ata kucha ukutane na radha mbaya ya rangi au hina 


Pia waweza kujipiga picha kucha uone jinsi kucha zako zilivokuwa mbaya sababu ya kuzing'ata...halafu baada ya majaribio hayo hapo juu upige tena uone zinavyopendeza na kuvutia hii itakusaidia uache iyo tabia.



        Challenge yourself: Ni muda gani unaweza kukaa bila kung'ata kucha? halafu ukiona umefanikiwa kakaa masaa kadhaa Then jitahidi sasa umalize siku nzima ,siku tatu,wiki moja  na ya pili na ndipo unaweza kujikuta umeacha kabisa tabia hiyo.

MIMI  NIMESHAANZA ZOEZI HILI NA WEWE PIA CHUKUA HATUA KAMA UNA UGONJWA HUU





No comments:

Post a Comment

HTML tags

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...