WAKATI utafiti ukiendelea kufanyika duniani kuhusu masuala ya afya,
suala la ubora wa maziwa kiafa nalo limeangaliwa kwa makini. Ni ukwel
ulio wazi kuwa watu wengi wamekuwa wakiambiwa kuwa maziwa ni miongoni
mwa vinywaji bora kwa binadamu na kwamba ndiyo chimbuko pekee la madini
aina ya ‘kashiamu’. Hata hivyo, siyo tu maziwa huwaletea madhara baadhi
ya watu, bali imegundulika ni chanzo cha magonjwa.
MAZIWA YA MAMA KWA WATOTO
Maziwa ya mama ndiyo chakula bora kwa mtoto mchanga kuliko kitu
kingine. Vile vile siyo tu maziwa ya mama ni bora kwa mtoto, bali pia
vilivyomo ndani ya maziwa hayo ni vya kipekee na haviwezi kupatikana
katika vyakula vingine. Kwa maana hiyo maziwa ya mama ni maalum kwa
mtoto tu.
Viumbe vinatofautiana namna vilivyoumbwa. Kwa mfano,
Ng’ombe anapozaliwa hadi kukua huchukua muda wa mwaka mmoja kukomaa
kimwili. Binadamu huchukua muda wa miaka 16 au zaidi kufikisha umri wa
kukomaa kimwili, ikiwa ni pamoja na kubalehe kwa mtoto wa kike au kiume.
Hii ina maana kwamba virutubisho vilivyomo kati ya jamii ya viumbe
fulani ni tofauti na jamii nyingine.
Mtoto anapoanza kukua,
mazingira ya tumbo nayo hubadilika ambapo huanza kulishwa vyakula vigumu
kiasi na idadi ya vyakula anavyolishwa huongezeka. Hata hivyo, wengi wa
watoto wanapoanza kupewa maziwa ya kopo huanza kuharisha, wengine
hufunga choo kwa siku kadhaa na wengine hushindwa kuyanywa kuonyesha
kutokubalika mwilini.
CHANZO BORA CHA ‘CALCIUM’
Mboga za majani
ya kijani ni miongoni mwa mboga zenye kiwango kikubwa cha virutubisho
vingi, vikiwemo ‘amino acids’, ‘omega 3’ na nyingine nyingi. Aidha,
mboga za majani zinaelezwa pia kuwa chanzo kizuri cha madini ya
‘calcium’ na ‘magnesium’ ambayo husaidia ukuaji wa mifupa mwilini. Hivyo
siyo lazima kunywa maziwa tu ili kupata madini hayo.
TAHADHARI MAZIWA YA PAKETI
Kwa mujibu wa watafiti wengi, maziwa ya paketi, ambayo kitalaamu
hujulikana kama ‘Pasteurized Milk’ au ‘Homogenized Milk’, huwa ndiyo
chanzo cha magojwa mengi. Kwa kawaida maziwa ya paketi hupitia hatua ya
uchemshwaji kiwandani ili kuua vijidudu vinavyosababisha kifua kikuu
(tuberculosis).
Pamoja na kupitia hatua hiyo kwa lengo la kuua
vijidudu, lakini virutubisho muhimu vilivyomo kwenye maziwa navyo
hupotea kutokana na joto kali linalotumika kuchemshia. Katika kujua
madhara ya maziwa ya paketi, utafiti ulifanywa ukihusisha watoto 70
ambao walipewa maziwa mabichi kwa muda wa miaka mitano ni mmoja tu kati
yao ndiye aliugua, lakini idadi hiyo hiyo waliopewa maziwa ya paketi, 14
waliugua!
Dk. Kurt Osler ni daktari bingwa wa moyo (Cardiologist)
kutoka Jimbo la Connectcut nchini Marekani na amekuwa akifanya utafiti
kuhusu maziwa ya paketi kwa muda wa zaidi ya miaka 20. Utafiti wake
umeonesha kuwa maziwa ya paketi (homogenized milk) husababisha kolestro
mbaya mwilini.
Dk. William Ellis ni mtaalamu wa mifupa, naye katika
utafiti wake ameona kuwa maziwa yanahusika kwa kiasi kikubwa na magonjwa
mbalimbali kwa watoto na watu wazima, kama vile uchovu, upungufu wa
damu, maumivu ya tumbo, kuharisha, magonjwa ya moyo na mzio (allergies).
Watafiti kuhusu ubora wa maziwa wameeleza kuwa kama kweli maziwa ya
ng’ombe yangekuwa ndiyo chanzo bora cha madini ya ‘calcium’, basi
ugonjwa wa mifupa usingekuwepo kwenye maeneo ambayo watu hunywa maziwa
kwa wingi, badala yake hali imekuwa kinyume.
Kwa ujumla, kama ilivyo
hata kwa vyakula vingine, maziwa ni miongoni mwa vinywaji vinavyotakiwa
kutumiwa kwa uangalifu na kwa usahihi, kinyume na dhana potofu
iliyojengeka miongoni mwetu kuwa maziwa hayana madhara yoyote kwa
binadamu.
No comments:
Post a Comment
HTML tags