Friday, August 5, 2011

Bundi mnyonya damu a.k.a Vempire

Bundi ni Mamalia  pekee wanaoruka,lakini Bundi wanyonya damu (Vempire) wana sifa ya pekee kabisa  ambapo chakula chao ni damu .


Bundi hawa wakiwa wadogo hawanyonyi damu bali hunyonya  maziwa ya mama zao  kwa miezi mitatu ndipo huanza kunyonya damu.

Bundi hawa hulala mchana kutwa na usiku kucha huwa mawindoni.Ng'ombe na punda waliolala huwa waathirika wakubwa, ila imefahamika kuwa  wakati mwingine Bundi hawa hunyonya damu za binadamu pia.  

Bundi hawa hutumia dakika 30 kunyonya damu ya kitoweo alichokipata.Ikitokea bundi huyu kakung'ata unaweza kupata maambukizi ya magonjwa yaliyomo mwilini mwake.



Bundi hawa  hupatikana kwa wingi nchini Mexico,Amerika ya kati na Amerika ya kusini.

No comments:

Post a Comment

HTML tags

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...