Tuesday, September 27, 2011

Mwanamke afunga ndoa na mbwa Accra, Ghana




NA: HAMIDA HASSAN 
Dunia hadaa ulimwengu shujaa! Ilishaelezwa kuwa ukishangaa ya Musa utastaajabu ya Firauni, tukio la mwanamke kufunga ndoa na mbwa lina rangi ya peke yake.

Emily Mabou, 29, amefunga ndoa na mbwa wake kipenzi na kwa mujibu wa madai yake, amefanya hivyo kutokana na mateso ya wanaume.

Hata hivyo, mshangao wa wengi upo kwenye maeneo mawili, mosi, binadamu kufunga ndoa na mnyama, pili, mbwa mwenyewe ambaye mdogo, kwani ana umri wa miezi 18 tu.

Ndoa hiyo, ilifungwa kimila na mfungishaji ni mtu mwenye mamlaka ya kisheria ya kufungisha ndoa.

Awali, ndugu zake walikuja juu na kumtaka asifanye hivyo lakini Emily alisisitiza kwamba ni lazima aolewe na mbwa wake kwa sababu ndiye mwenye sifa zote anazohitaji kutoka kwa mwanaume.

Alisema, siku zote amekuwa akitamani kumpata mwenzi wa maisha kutokana na wanaume wengi kuwa hawaamini.

“Baada ya uchunguzi wangu, nilibaini huyu mbwa ndiye mume wangu wa kweli. Ana mapenzi ya dhati na anaweza kuniridhisha kimwili na kunikamilishia furaha yangu,” alisema Emily.

Aliendelea kusema: “Nimekuwa nikiomba nimpate mwanaume mwenye sifa zote kama alizokuwa nazo baba yangu. Baba yangu alikuwa mwema, mkarimu na mkweli kwa mama yangu na hakuwahi kumtendea mabaya.

“Nimekuwa kwenye mapenzi kwa muda mrefu na wanaume mbalimbali, wote ni sawa tu, wanapenda sketi halafu ni wadanganyifu kupitiliza.
Mbwa wangu ni mzuri, na ni mkweli kwangu na amekuwa akiniheshimu sana, kwa hiyo anastahili mapenzi yangu, anafaa kunioa, niwe mke naye awe mume.”

Hata hivyo, kaka wa Emily, David Mabou alisema kuwa familia yao ilimtenga mrembo huyo kwa sababu alichokifanya siyo heshima kwa jamii.

“Ni ndoa ya kishenzi, amewadhalilisha wanaume wote na ameukana ubinadamu wake, tangu lini binadamu akafunga ndoa na mnyama? Aibu kwake, ameiudhi sana familia yetu,” alisema David.

Wakati wa kufunga ndoa hiyo, msimamizi wa shughuli nzima aliwataka watu wasiicheke harusi hiyo wala kuikebehi, bali washerehekee na kumpongeza Emily kwa kupata furaha ya kudumu.

No comments:

Post a Comment

HTML tags

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...