SOMENI, WARAKA WANGU KUTOKA IGUNGA.
NILICHOKUWA NIKIFIKIRIA KUHUSU IGUNGA: Nilichokuwa nikiamni kuhusu igunga bilashaka hata wewe, ni kuwa Igunga ulikuwa mji wenye mafanikio na maendeleo makubwa hasa kutokana na kile tulichokuwa tukisikia mbunge aliyetangulia alikuwa akikifanya.
REALITY: Ukweli ni kwamba hali ni tofauti kabisa, ukisuka stendi utakutana na vijana waliochoka maisha wakiwa wanapiga
soga roadin…kasha unakutana na vumbi kubwa la barabaraba ukiondoa lami ya higway kuelekea Mwanza na shinyanga, baadae ukitaka kuoga ndio kabisa utakutana na maji yenye mfano wa maziwa yaliyotiwa majani ya chai. Kiufupi maendeleo ni kidogo sana kuliko hali halisi iliyokuwa ikiripotiwa.NILICHOKUWA NIKIFIKIRIA KUHUSU IGUNGA: Nilichokuwa nikiamni kuhusu igunga bilashaka hata wewe, ni kuwa Igunga ulikuwa mji wenye mafanikio na maendeleo makubwa hasa kutokana na kile tulichokuwa tukisikia mbunge aliyetangulia alikuwa akikifanya.
REALITY: Ukweli ni kwamba hali ni tofauti kabisa, ukisuka stendi utakutana na vijana waliochoka maisha wakiwa wanapiga
ILIKUWAJE MBUNGE AKAWA ANATEULIWA?: Kuhusu hili sitaki nisemem mengi kwakuwa yapo mengi pia yanayosemwa kuhusu hili. TAFAKARI!!!
KUHUSU DSTV NDIO NILICHOKA KABISA: Suala la DSTV lilikuwa kituko kwangu, eti wananachi walimlalamikia mbunge kuwa wanataka kuona ligi za ulaya, na mbunge bila hiyana akwanunulia BIG SCREEN ambayo hata mimi nilishuhudia mechi moja nikiwa kazini kufanya uchunguzi..teheteheteheteheteh
MWENENDO WA KAMPENI ZILIVYOKUWA: Kampeni zilikuwa za wenye fedha kuweza kuteka wananchi wengi zaidi, kwa vile vyama vya akina kajamba nani basi unapiga mikutano miwili umemamiliza, mfano mzuri ni mgombea wa UPDP, alifanya mkutano wa ufunguzi na kufunga biashara ikaishia hapo. Kuhusu miamba mitatu CUF, CHADEMA na CCM mwendo ulikuwa wa Helkopta, fedha zilimwagwa kwa wapiga kura, wapo wazee niliwashuhudia wakileweshwa ili wasiende kupiga kura huku wengine wakipigiwa kura zao. Kubwa ya yote ni kuona chama cha CCM kupitia kwa katibu mkuu wake Wilison Mukama kulalamika kuwa watendaji wa serikali waliokuwa wakisimamia uchaguzi huo eti waliibeba chadema?????
KUHUSU UANDISHI WETU: Wapo waandishi waliotuponza tukaanza kusakwa na wananchi wa Igunga kwa kutoa habari zisizo sahihi shukrani kwa jeshi la Polisi kwa kutupa ulinzi. Ila nachotaka kusema hapa hatuan awaandishi, waandishi wengi walinunuliwa na vyama vya siasa na kusahahu maadli ya kazi zao.
MTAZAMO WA WANANCHI KUHUSU MBUNGE MPYA: Wananchi wanamatumaini huenda mbunge mpya akasaidia kuleta maendeleo kwa kile walichoeleza ni ushindi wa tofauti ya kura chache walizopishana na CHADEMA.
UTENDAJI WA JESHI LA POLISI: Kwa mara ya kwanza nimeshuhudia polisi wakifanya kazi kwa heshima ya juu ya utii wa haki za binadamu, waliopigwa ni wale waliozidisha furaha ama vurugu, walikuwa fair kiasi ambacho hata CCM walihisi kana kwamba jeshi la polisi linawaunga mkono CHADEMA lakini sihivyo. Nalipongeza jeshi la Polisi kwa kazi nzuri waliyoifanya Igunga.
HITIMISHO: Hitimisho ni kuwa CHADEMA wakubali matokeo kwani wamejitahidi sana ukizingatia ni mara yao ya kwanza kusimamisha mgombea, japo wengi wanaamini wizi ulikuwepo hilo linajulikana. Kupaa kura elfu 23 kati ya elfu 26 za CCM si haba. Kuhusu CUF ni lazima wajipange upya endapo wanataka kushindana na CCM na CHADEMA vyenye nguvu sana sasa.
No comments:
Post a Comment
HTML tags