Wednesday, November 16, 2011

BINADAMU AGEUKA MTI

Ama kweli hujafa hujaumbika,Nimesoma stori hii kwenye gazeti la uwazi na imenigusa kweli kweli. 
Huyu ndugu anaitwa Dede Koswara (41) raia wa Indonesia hivi sasa hatamaniki kwasababu ni nusu mtu nusu mti baada ya kushambuliwa na virusi viitwavyo papilloma(HPV) ambavyo vimebadili kabisa muonekano wake.
Dede amekaa na ugonjwa huo takribani miaka 24 sasa na alishafanyiwa upasuaji mara kadhaa lakini tatizo liko palepale.
Mwenyewe bado ana matumaini  ya kupona ugonjwa huo na anatamani sana kuoa ili aje awe baba wa familia siku moja.
Nami naamini MUNGU atakuponya,endelea kushikiria imani yako tu.



No comments:

Post a Comment

HTML tags

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...