Kama ilivyo kwa watu wengine wengi, mimi pia ni mmoja kati ya watu ambao huwa napokea text nyingi za kufowardiwa kama ninavyoziita mie.
Mwezi uliopita nilipokea nyingi sana kutoka kwa marafiki, jamaa na ndugu pia,kuna baadhi ambazo zilinibamba kweli kweli kiasi kwamba huwa nazisoma mara kwa mara kadri ninapopata muda wa kufanya hivyo.
Zifuatazo ni baadhi ya hizo text zilizonibamba
ZA KIMAISHA- Sasa nimegundua DAWA YA MAISHA ni kulipiza kisasi, ukinichukia nakupenda, ukiniudhi nakufurahisha, ukinisahau nakukumbuka, ukikaa kimya nakusalimia,Mambo vipi?
- Leo nakupa practical QNS chukua 259 zidisha miaka yako ,jibu upatalo zidisha 39, utapata tarakimu 6, ambapo kila tarakimu mbili zitamaanisha miaka yako. testi uone.
- Wazaramo bana...noma, wamemkamata mwizi hawajampiga wala kumpeleka polisi... wakamsema mpaka akazimia.
- Nasikia ulikuwa unaumwa,ukaamua kuweka picha ya Daktari kwenye ukuta wa chumba unacholala,ukiulizwa kwanini umeamua kuiweka ukutani picha ya daktari?ukajibu nimeambiwa maumivu yakizidi nimwone daktari.
- Uzuri wa Yusufu haukumfanya ajivune,utajiri wa Suleimani haukumsahaulisha ibada,maradhi ya Ayubu hayakumfanya akufuru,kufungwa 2mbo kwa Sara hakukumfanya aache kumwamini MUNGU,kupigwa kwa Stefano hakukufanya amkane mungu..je hali tulizonazo zinampaje MUNGU utukufu?
- MUNGU na akupe hekima kama za Suleimani,akupe imani thabiti kama ya mtumishi wake Ayubu,akulinde kama Danieli katika tundu la simba,akupe ujasiri kama wa Samsoni dhidi ya wafilisti,akuhifadhi kama Yona katika tumbo la samaki,akunusuru kama alivyomnusuru Nuhu na gharika kuu,na akupe ushindi kama wa Musa dhidi ya Farao,akubariki kama alivyombariki Ibrahimu na akujaalie neema kama alivyomjaalia Mariam.
- I want you to know that I love you so much!mic u big!
- Got a problem?,got GOD, then u've got a solution.
*Kuandika kwa vifupisho ndio mpango mzima...na kama huvijui ndio imekula kwako
Texts hizi ni nzuri sana, maana huwa zinafundisha,kutia moyo,kufurahisha na hata wakati mwingine zinabore kwani unaweza kupata text ya aina moja kutoka kwa watu watano tofauti.
Ukitaka kudelete, basi cheki kwanza imeandikwaje maana kuna watu wengine wakiiona mwanzo tu kama ni text ya kufowardiwa wanadelete fasta bila hata kuisoma...usifanye hivyo bana
Najua umenisoma...
with love
DeBonex.
No comments:
Post a Comment
HTML tags