Tuesday, August 23, 2011

Tunawatunzaje wazee wetu?

Kuwatunza wazee si jambo rahisi na watu wengi hulikwepa hasa pale inapotokea kuna mzee hapo nyumbani wanapoishi.



Kukosa watu wa kuwatunza ni tatizo kubwa linalowakabili wazee ambao wamefikia hatua ya kutoweza kujitunza wao na nyumba zao.
Mbali na pesa na vitu kama nguo,chakula n.k watu hawa huitaji watu wa kuwatunza, kwasababu wengi wao wanakuwa hawana uwezo wa kufanya shughuri kama ilivyokuwa zamani enzi wakati wana nguvu zao labda kutokana na umri wao kwenda sana na wakati mwingine magonjwa yanayowakabili.


Swali la kujiuliza, kama una mzee nyumbani kwako je ni nani anayemtunza na kumuhudumia??
Ikumbukwe kuwa si kila mtu anaweza kuhudumia mzee,watu wengi huweza kuhudumia watoto lakini si watu wenye special need kama wazee.
Watu wengi hupenda kuhudumia wazee ambao kwa namna moja au nyingine wana undugu nao...sasa tuwe makini na wasaidizi  tunaowaachia watutunzie wazee wetu.


Maisha ni kutunzana kama ambavyo tumetunzwa tukiwa watoto na sasa yatupasa kuwatunza walio wadogo kwetu na zaidi sana ni wazee tulionao ili nasi tuje tutunzwe pale tutakapofikia hatua ya kuzeeka.




Daima tujifunze kuwaambia wazee wetu, "I love you" na pale tunapokosea  tuwaaambie"Forgive me",  ili tuzidi kupata baraka zaidi na zaidi.




No comments:

Post a Comment

HTML tags

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...