Saturday, December 29, 2012

muda mrefu umepita na mwaka umekaribia kuisha...

Mwendelezo...

Kwa habari ya wale wanaoomba msamaha kama mazoea,hakikisha mwaka 2012 ndio mwisho ifikapo mwaka 2013 uwe unamaanisha kila unachosema kama nimsamaha uwe umekusudia kubadilika kweli.

Najua kuna mambo/matukio mengi ambayo yatakuwa yamekuumiza mwaka huu 2012,usijali hayo yamepita na kama msemo wa wahenga usemavyo yaliyopita si ndwele tugange yajayo,basi tutegemee mambo mema na ya baraka zaidi katika mwaka ujao.

Katika siku chache zilizobakia,nawasihi tuzitumie kumshukuru MUNGU kwasababu anatupenda sana ndio maana tunaishi mpaka leo hii...sio kwamba sisi ni wazuri sana au kwamba sisi tunafaa sana bali ni mapenzi yake MUNGU baba yetu na ana makusudi na maisha yetu.

Kumbuka watu waliokuwa katikati yetu wakiendelea na maisha yao kama kawaida walikufa ghafla bila kufikia malengo yao tena wengine wakiwa vijana ,sitaki kuwakumbusha machungu lakini msiba wa Kanumba ni mfano mzuri sana katika hili ninaloliongelea,sio kwamba sisi tunafaa sana zaidi yake tuendelee kuishi hapa duniani...la hasha ni upendeleo wa MUNGU tu.

Nawasihi tuendelee kutunza kumkumbuka muumba wetu na kumtumikia kila wakati kwani sie ni wapitaji tu hapa duniani na safari yetu ni moja sote twaijua hivyo tusijasahau na kujiachia sana(ushauri wa bure).

Najua umezoea kuona naweka picha nyingi,lakini nimejisikia kuongea zaidi na wewe mwana Afroshiznet tunapoelekea kuumaliza mwaka huu.

Nimeongea mengi lakini all in all naomba mwaka 2013 mzingatie suala la kumkumbuka MUNGUna katika blog hii kutakuwa na mambo mengi ya kuvutia na vitu vingi vya ubunifu utavipata hapa hapa Afroshiznet .

Nawatakia heri ya mwaka mpya 2013 na mafanikio tele.

Endelea kutembelea afroshiznet blog.

De Bonex.

No comments:

Post a Comment

HTML tags

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...