Friday, December 28, 2012

Muda mrefu umepita na mwaka unakaribia kuisha...

mpendwa mdau wa afroshiznet,

ni matumaini yangu uko fresh kabisa
hatujaonana muda mrefu kidogo, lakini kama mjuavyo majukumu ni mengi so wakati mwingine muda unakuwa mchache kuingia pande hii...

lakini kabla ya mwaka kuisha ni vyema tukapata tathmini ya mambo na matukio mbalimbali ya mwaka tunaoelekea kuumaliza.

mie kwangu ulikuwa mwaka mzuri kwani asilimia 80 ya malengo yanngu yalitimia,kwakweli nimemuona MUNGU natumaini na wewe pia mambo yako yalifanikiwa, maana MUNGU anatuwazia mema siku zote.

sikumbuki kuwa na ugomvi au kinyongo na mtu yeyote ingawa mimi ni mwanadamu kama wanadamu wengine so  ninaweza kuwa nimejikwaa na kumkwaza mtu mahali fulani muda fulani,naomba tusameheane sana.

kumekuwa na kasumba ya watu kupenda kuomba misamaha ifikapo mwisho wa mwaka lakini utakuta mwaka mwingine unavyoanza mambo yanakuwa yaleyale.

basi,wanaafroshiznet nawaasa kuwa makini na tayari kutendea kazi maneno tunayozungumza.

itaendelea...


No comments:

Post a Comment

HTML tags

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...